Nafasi za kazi 24:Watu wa masoko na madaktari wa mifugo | MASWAYETU-BLOGSPOT
Breaking News
Loading...

Sunday, December 18, 2016

Nafasi za kazi 24:Watu wa masoko na madaktari wa mifugo

BONYEZA HAPO CHINI KUJUA KUHUSU LINI AJIRA ZA WALIMU 2015/2016 ZITATOKA
Shirika la Tanzania Youth and Entrepreneurship Organization (TYEEO) lenye usajili namba 00NGO/00006706.

- Shirika la TYEEO,limeanzisha miradi mikuu miwili,

(i) Mradi wa kutotoresha vifaranga uliofungwa mitambo yake kisarawe mkoani pwani ambapo itazalisha vifaranga zaidi ya 40000.

(ii) Mradi wa ufugaji kuku katika shamba kubwa litakalo fuga kuku zaidi ya 60000,katika eneo la homboza chanika Dar es Salaam.

-Kupitia miradi hii miwili shirika linapenda kutangaza nafasi za kazi zifuatazo:-

1.Watu wa masoko nafasi 15

Sifa za mwombaji

-Awe na elimu ya masoko(Marketing ), kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada

-Awe na uwezo mzuri wa kujieleza na kuelezea bidhaa.

-Awe na umri kati ya miaka 22 hadi 26

-Awe tayari kufanya kazi ndani na nje ya ofisi

-Awe na jinsia ya kike

Majukumu ya mtu wa masoko

-Kutafuta masoko ya bidhaa zitakazo kuwa zinazalishwa na mradi kama vile kuku,mayai na vifaranga, kwa kutembelea maofisi mbalimbali na kwa njia ya mtandao yaani internet.

-Kushawishi wafugaji binafsi wa kuku kujiunga na mradi wa ufugaji wa pamoja kwa kuwaelezea faida zake kiuchumi na kibiashara.

1.Madaktari wa mifugo nafasi 9.

Sifa za mwombaji

-Awe na elimu ya mifugo , kuanzia ngazi ya stashahada hadi shahada

-Awe na uzoefu wa kutibu kuku au awe amewahi kufanya kazi katika miradi ya ufugaji kuku.

-Awe na umri kati ya miaka 22 hadi 28

-Awe tayari kufanya kazi ndani na nje ya ofisi

-Awe na jinsia ya kike

Majukumu ya daktari wa mifugo

-Kutoa chanjo na dawa kwa kuku.

-Kusimamia na Kufatilia afya za kuku waliopo katika mradi na kwa wateja wa nje wa shirika

-Kutibu na kupambana na magonjwa yatakayo jitokeza katika eneo la mradi wa kuku na kwa wateja.

-Kutoa ushauri wa kuboresha mazingira ya kiafya ya kuku

-Kutoa ushauri wa kitabibu kwa wafugaji wapya na wazamani watakao kuwa wanatembelea ofisi zetu.

-Kushirikiana na watu wa masoko ili kufikisha elimu sahihi ya ufugaji kuku kwa wadau.

Namna ya kutuma maombi

Barua zote za maombi ziletwe kwa mkono ofisi za TYEEO kuanzia tarehe 19.12.2016 saa mbili asubuhi na mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 22.12.2016 saa kumi na moja jioni.

Ambatanisha vitu vifuatavyo:-

-Vyeti vyako vyote vya taaluma kuanzia kidato cha nne

-Curriculum vitae

-Cheti cha kuzaliwa

-Barua yako ya maombi ya kazi

MAHALI OFISI ILIPO

Ukishuka stand ya Gongolamboto utakuta ghorofa ndogo nyeupe ina bango kubwa la kuku limeandikwa TYEEO CHICKEN PRODUCTION.


Block No. 370 – 2BLOCK E SECOND FLOOR

Au piga simu namba
Hotline No: 0657-115587.

Ukifika ulizia ofisi za kuku,ipo floor ya pili.

Wote ambao watafanikiwa wataitwa kwenye usaili tarehe 30/12/2016 saa mbili asubuhi. v

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT

     


    Travel

    About Us