Tangazo la nafasi ya kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho katika Manispaa ya Temeke na Kigamboni. | MASWAYETU-BLOGSPOT
Breaking News
Loading...

Tuesday, December 27, 2016

Tangazo la nafasi ya kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho katika Manispaa ya Temeke na Kigamboni.

BONYEZA HAPO CHINI KUJUA KUHUSU LINI AJIRA ZA WALIMU 2015/2016 ZITATOKA

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA KUKUSANYA USHURU WA MAEGESHO KATIKA MANISPAA YA TEMEKE NA KIGAMBONI.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam anawatangazia wakazi wa Dar es Salaam wenye sifa, nafasi ya kazi ya kukusanya mapato ya maegesho katika  Manispaa ya Temeke na Kigamboni jumla ya Nafasi Sitini (60). Kazi hii itakuwa ni ya Mkataba wa miezi mitatu na mshahara utalipwa kwa kuzingatia Sheria ya Ajira Cap. 300 “Wage Order” 2013 ambao utakuwa sh.150,000/= kwa mwezi.
SIFA ZA MWOMBAJI:
·   Awe Raia wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na umri usiozidi miaka 60
·   Awe na elimu ya darasa la Saba na kuendelea
·   Awe na uwezo wa kutumia “Smart phone” katika miamala ya malipo
·   Awe na Uzoefu usiopungua miezi sita katika masuala ya kukusanya Ushuru.
·   Awe mwadilifu na mwaminifu na awe hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai
MAELEKEZO YA JUMLA
·   Waombaji waambatishe vivuli vya vyeti vya taaluma zao pamoja na cheti cha kuzaliwa
·   Kila barua ya muombaji iambatishwe na picha moja ndogo (Passport size) iliyopigwa siku za karibuni.
·   Barua ya Maombi iambatishwe na:
- Barua kutoka kwa wadhamini wawili ambao ni watumishi wa Serikali zikiwa na picha “Pass port size” ya hivi karibuni, Anuani kamili ya  makazi, pamoja na namba zao za simu.
- Barua ya Utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa.

- Wasifu (CV)
·   Waombaji watakaokuwa “Shortlisted” watajulishwa kwa njia ya simu tarehe ya usaili.
·   Barua ya maombi ya kazi iletwe kwa njia ya mkono katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuanzia tarehe ya tangazo hili au kwa njia ya posta kupitia anuani tajwa hapo chini kuanzia saa mbili kamili (2:00) asubuhi hadi saa 8:00 mchana.  Mwisho wa kupokea maombi ya kazi ni  tarehe 27 Disemba, 2016 saa 8:00 mchana.
Maombi yatumwe kwa Anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi wa Jiji,
Halmashauri ya Jiji,
Ukumbi wa Jiji,
1 Barabara ya Morogoro,
S.L.P. 9084,
11882 – DAR ES SALAAM

Tangazo hili pia linapatikana kwenye tovuti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo ni www.dcc.go.tz
Sipora J.Liana
MKURUGENZI WA JIJI  
HALMASHAURI YA JIJI LA DAR-ES-SALAAM
v

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT

     


    Travel

    About Us