Hofu na woga ni adui mwingine wa kuthubutu kuanza
biashara. Ili uweze kuwekeza katika biashara tanguliza kujifunza upate ujuuzi
kidogo wa kuanzia unachotaka kufanya, ikiwa utaona fursa inaweza kubadili
maisha yako mbeleni, weka nyuma hofu na
woga wa kupoteza pesa, usiache fursa ikupite huku ukiwa unahitaji.
Chanzo cha hofu
Hofu huanza pale unapotafuta usahihi. Unataka asilimia mia usikosee, upate
matokeo chanya kwa kitu unachotarajia kufanya katika biashara. Hakuna biashara
ambayo itakuhakikishia mafanikio asilimia 100 bila hatari yoyote.
MAISHA HALISI
Katika maisha halisi na biashara, hatuna usahii, tunakufanikiwa na kushindwa
basi. Usahihi wa kutaka ufanye vitu sawa sawa kabisa bila kukosea mahali pake
ni shuleni unapokuwa darasani. Katika ulimwengu wa biashara usiogope kushindwa,
ogopa kuacha kujaribu.
Katika maisha
tunajifunza hatua kwa hatua kwa vitendo bila kujali utakosea, kwa sababu mafanikio katika maisha halisi hayapatikani
kwa kufanya nadharia. Nimeona napomfundisha watu kuhusu biashara ya mtandao,
baadhi wanataka wajifunze kila kitu ndio waanze, mimi huwa nawambia hiyo ni
hofu ya kushindwa. Katika biashara haipo siku utasema nimejifunza kila kitu
kwenye biashara yangu. Kila siku unajifunza na biashara yako inakuwa. Elimu ni
bahari.
Hata tungepewa muda, nikakufundisha kwa nadharia
maisha yako yote ya muda wako hapa duniani, kisha ukapewa muda sasa wa kuanza safari ya mafanikio kwa
vitendo bado utaanguka na biashara itakufa au utachukua muda mrefu kupata
mafanikio mfano wa punje ya ulezi.
Maisha ya duniani nitofauti kabisa na darasani. Huku
unahitaji mbinu za kufanikiwa kimaisha na muda mwingine zinapingana kabisa na
ulichofundishwa darasani. Usibebe darasa lote ukaleta huku maisha yatakuwa
magumu, na utaendelea kuona wasio na elimu za juu wanaendelea kuneemeka.
Wataneemeka kwa sababu wanafuata taratibu za mafanikio katika maisha
zinazotumika huku, wewe unalazimisha principle za mafanikio ya darasani
zitumike na huku.
Soma: IFAHAMU TABIA INAYOKWAMISHA MAFANIKIO YAKO
Kuwa mkufunzi wa hii biashara ya mtandao kumenifanya
nijifunze mengi kutoka kwa baadhi ya wasomi, kwa kifupi niseme bila kuacha
majivuno, kujiona kuwa una MBA, BBA n.k ndio kila kitu bado utasota sana hasa
kama umetokea familia ya daraja sawa na langu. Kama kuwa na elimu kubwa ya
darasani ndio mafanikio makubwa kiuchumi, dunia ingekuwa inaongozwa wasomi
wakubwa kwa mafanikio, let us change our mind.
Kuna uhusiano wa hofu katika kuanza biashara na mtu anayetumia
elimu ya darasani kupata mafanikio, anayetumia elimu ya darasani huhitaji
usahihi mkubwa kwa kila jambo yaani anataka kama ikivyokuwa darasani akipewa
mtihani apate daraja A au B+.
Mtihani katika maisha halisi ni mafanikio ya kile
unachokifanya hivyo kama unaogopa kuanza katika vitendo ujue unaogopa
kufanikiwa, huwezi fanikiwa katika biashara kwa nadharia, yaani uendeshe biasha
kinadharia mi sijui faida yake utaipataje. Hivyo lazima uanze ndio mafankio
uyaone vinginevyo utakuwa unataka ujifunze kwa nadharia na maisha hayana
nadharia ukijfunza kwa wa nadharia na maisha yanakuwa nadharia. Jifunze kwa
vitendo.
KUPUNGUZA HATARI YA KUPOTEZA MTAJI.
Usiogope kuanza biashara, kama hofu ni kupoteza pesa
yako, ili kupunguza hatari ya kupoteza mtaji, jitihada na muda wako tathimini
biashara yenyewe ikiwa utaona itakupa mafanikio mbeleni na kukufanya uishi
maisha unayotaka badae basi jua inamafanikio, anza kuangalia jinsi utakavyoweza
kuimiliki hiyo biashara na kuiendesha na kufikia mafanikio.
Usijiwekee vikwazo kufikia mafanikio, nilikuwa
katika hali ngumu ya kifedha wakati naanza biashara katika mfumo wa biashara ya
mtandao (MLM); nilikuwa nafundisha shule binafsi, lakini ulipaji wake ulikuwa
shida inapita hadi miezi miwili bila mshahara na wakilipa wamalipa nusu hadi
naondoka niliacha pesa zangu, hii ilifanya nishindwe pale ninapopata mshahara
kupanga kufanya vitu mhimu vya kimaendeleo kwa sababu nashindwa kujua lini tena
nitalipwa.
Mwisho niliona hiyo haisadii, nilifikria ni biashara
gani nifanye lakini bila kuacha kazi na kwa mtaji kidogo, nilifkria fursa
nyingi lakini mwisho nikapata fursa ya biashara ya mtandao.
Ukitaka kuanza biashara na ukasilikiliza
walioshindwa na wewe unakuwa unaongeza nafasi ya kushindwa, vinginevyo uweke
akili yako katika mtizamo chanya unapowasikliza. Changamoto nilizosimuliwa
katika hii biashara zilikuwa, za kukatisha tamaa, nashukuru MUNGU nilizizika
shimoni. Baada ya kuona mbele, nikaona ikiwa nitazikabili changamoto zote
walizonambia nitapata nachokitaka mbeleni, nilipata nguvu ya kuanza. Nilijua
hakuna biashara nitakayoanza ikawa haina vikwazo vinginevyo nifie katika ajira
nikistafu nile kinua mgongo.Niliona
nachotakiwa ni kuondoa vigingi vyote nitakavyokutana navyo na mwisho
ntafikia mafanikio. Nashukuru Mungu kwani hadi sasa, nimeongeza chanzo cha
kipato, timu yangu inazidi kukua, nimeweza kuwa na website ambayo najua badae
nayo itakuwa ni chanzo kingine cha kipato na nguzo ya biashara yangu. Kuwa
mjasiriamali kuna hitaji ujasiri.
Waliofanikiwa wote katika biashara walifumba macho
na kuangalia mbele, walianguka kibiashara lakini walijua kuna mafanikio mbele,
waliamuka na kuanzia walipoishia. Nakusihi ndugu yangu rafiki na msomaji wa
makala hii, weka uoga nyuma anza sasa.
v
0 comments:
POST A COMMENT