Rais Magufuli apigilia msumari Sakata la Madawa ya Kulevya......Ataka Polisi Wasiangalie Umaarufu wa Mtu, Asema hiyo sio Vita ya Makonda Pekee | MASWAYETU-BLOGSPOT
Breaking News
Loading...

Monday, February 6, 2017

Rais Magufuli apigilia msumari Sakata la Madawa ya Kulevya......Ataka Polisi Wasiangalie Umaarufu wa Mtu, Asema hiyo sio Vita ya Makonda Pekee

BONYEZA HAPO CHINI KUJUA KUHUSU LINI AJIRA ZA WALIMU 2015/2016 ZITATOKA




Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaohusika na Dawa za Kulevya bila kuangalia umaarufu au cheo cha mtu.

Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza  mara  baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Vanance Mabeyo pamoja na viongozi wengine wa majeshi, na mabalozi.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alianza kwa kumpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu kwa hatua nzuri aliyoichukuwa ya kuwasimamisha kazi Askari Polisi 12 waliotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya ili kupisha uchunguzi.

Rais Magufulia amesema hakuna wa kuachwa hata akiwa mkewe Mama Janet Magufuli, na kuongeza kuwa wakamatwe bila ya kujali majina yao.

"Najua IGP Mangu watu walikupigia simu wanakupa ushauri kuhusu Dawa za Kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa IGP.
"Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni.
"IGP nakuagiza kamata watuamiaji wote wa dawa za kulevya hao watakwambia wanapozipata, haiwezekani ziuzwe kama njugu."Amesema Rais Magufuli
Akizungumzia suala la uendeshaji wa kesi za dawa kulevya, Rais Dkt Magufuli amemwambia Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania,  Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa kesi hizo zinaendehswa taratibu sana huku akitolea mfano wa mfanyabiashara mmoja maarufu wa dawa za kulevya aliyekamatwa mkoani Lindi lakini hakuwahi kufikishwa mahakamani. 
"Kuna mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya alikamatwa mkoani Lindi lakini sijawahi kusikia amefikishwa mahakamani" Amesema Rais Magufuli.

Rais  Magufuli amesema kuwa vita ya dawa za kulevya si ya Paul Makonda peke yake bali ni ya Watanzania wote huku akivitaka vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama kushirikiana kutokomeza tatizo hili linalopelekea kupoteza nguvu kubwa ya taifa.
        
           by Gaspal simon mazengo


v

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT

     


    Travel

    About Us