Sakata la jenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Simiyu limeendelea kuibua mapya, ambapo Mhandisi wa ujenzi wa mkoa Deusdedit Mshuga amesimamishwa kazi na kufunguliwa mashitaka matatu ya kiutumishi.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kusimamishwa kazi kwa meneja wa wakala wa majengo ya serikali mkoa wa Simiyu (TBA) Michael Semfuko, kufuatia agizo la Rais magufuli la kutaka gharama za ujenzi huo zipunguzwe kutoka Bilioni 46.5 hadi Bilioni 10.
Akiongea na waandishi wa habari leo (jana) ofisini kwake Mkuu wa Mkoa huo Antony Mtaka alisema kuwa baada ya maagizo ya Rais iliundwa tume ambayo ilishirikisha kamati ya ulinzi na usalama mkoa pamoja na TBA.
Alibainisha kuwa tume hiyo imegundua kuwa mchoro wa ujenzi ambao alionyeshwa Rais Magufuli haukuwa wenyewe, bali ulikuwa ukionyesha vyumba vya madarasa, vyumba vya miskiti na makanisa.
“ ramani aliyoonyeshwa Rais magufuli juu ya ujenzi wa hospitali ya mkoa, ilikuwa siyo yenyewe, wataalam wetu walimdanganya Rais juu ya uhalisia wa ramani yenyewe ambayo ilikuwa ikikadiliwa kutumia shilingi Bilioni 46 kwa jengo moja la wagonjwa wan je (OPD)” Alisema Mtaka
Katibu Tawala wa mkoa huo Jumanne Sagini alisema kuwa kufuatia hatua hiyo ya mkuu wa mkoa kumsimamisha kazi mhandisi Mshuga ofisi yake imechukulia hatua za kinidhamu.
Alisema kuwa yeye kama mamlaka ya nidhamu ya watumishi sekretalieti ya mkoa tayari amechukua hatua za awali kwa kumfungulia mashtaka matatu ya kiutumishi ambayo alisema Mshuga atatakiwa kujibu ndani ya siku 14.
Aliyataja mashataka hayo kuwa ni kushindwa kutekeleza majukumu aliyopewa kwa kiwango cha kuridhisha kinyume na kipingele cha 8 sehemu A, Jedwali la 1, la kanuni za utumishi wa umma tangazo la serikali namba 168 , 2003.
Katika shtaka la pili kufanya uzembe mkubwa wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kazi aliyopewa kinyume na kipingele cha 13 sehemu A, Jedwali la 1, la kanuni za utumishi wa umma tangazo la serikali namba 168 , 2003.
Shtaka la tatu kufanya kazi kwa kukika maadili ya taaluma yake wakati wa majukumu yake kinyume na kipingele cha 14 sehemu A, Jedwali la 1, la kanuni za utumishi wa umma tangazo la namba 168 , 2003.
picha na Gaspal simon mazengo
MASWAYETU TEAM.
0 comments:
POST A COMMENT