Namna ya
kuandika CV nzuri, kila kitu kuhusu kuandika CV nzuri, andika CV nzuri upate
kazi nzuri, yote haya na mengine mengi katika Maswayetu Tanzania.
CV yenye
kujitosheleza ni njia muafaka ya kumfanya bosi wako mtarajiwa kukufahamu wewe.
CV nzuri inakupa nafasi ya kung’aa katika kikundi na kupata fursa ya usahili na
baadae kazi.
Pitia
matangazo ya kazi
Unapopitia
matangazo ya kazi katika magazeti, kuta za matangazo au barua pepe hakikisha
unapitia matangazo hayo kwa umakini. Fanya maamuzi ya kipi kati ya ujuzi, sifa
ama uzoefu utatumia katika kazi yako mpya.
Orodhesha vitu
hivi na tumia maneno yenye kuonyesha vitendo kwa mfano : Mimi ni mtu mwenye
mpangilio, ufanisi na mchapa kazi, nimeongoza na kusimamia watu na
matukio. Nimesoma na kufikia ubora
katika weledi na kumaliza shahada ya kwanza katika…..
Kua sahihi kwa kutoa maelezo mafupi yenye kueleweka
Usizidishe
maelezo kwa kutoa maelezo yote kukuhusu wewe, hakuna anayetegemea wala kutaka
kuyasikia hayo kwa hiyo usifanye hivyo.
CV inatakiwa
kumwelezea mtu lakini si kama kitabu kinachoelezea wasifu wako lakini pia si
aya/ibara ama kitabu unachoelezea hadithi ya maisha yako ya weledi! Hakikisha
huweki taarifa zako binafsi ambazo hazihusiani na nafasi unayoomba.
Sema
ukweli
Kua mkweli. Kwa
kufanya hivyo unaonyesha kujiamini na mafanikio yako na hii itakusaidia
inapokuja kukaa kwa ajili ya usahili. Huwezi kuzungumza kuhusu uzoefu wako kama
mwanasayansi wa nyuklia kama hukufaulu masomo ya sayansi shuleni!
Epuka
makosa haya
Vitu vichache
vya kuepuka kufanya: Usidanganye, usizidishe chumvi, usiweke ahadi usizoweza
kuzitimiza.
Vidokezo
katika kujielezea
Orodhesha
majumuisho yako.
Elezea CV yako
katika lugha chanya
Inasaidia kama
utaandika sentensi fupi na zenye kuonyesha uhai na kuepuka kutumia vivumishi
vingi.
Anza na
mafanikio yako ambayo yanawiana na mahitaji muhimu ya kazi. Usimweleze mwajiri
ni kwa vipi atakusaidia bali mueleze ni kwa vipi wewe utamsaidia.
Tia msisitizo
katika uzoefu unaohusiana na biashara ama kazi husika. Kama una uhusiano mzuri
wa kazi na wataalamu katika fani yako unaweza kuwaomba kuwatumia kama
wadhamini.
Pata ushauri
kabla hujatuma CV yako. Tafuta mtu unaemjua katika fani husika ili apitie CV
yako. Jiandae kurekebisha vitu ulivyoandika.
Jaribisha CV
yako kwa kuomba nafasi mbalimbali katika kiwango chako lakini pia kiwango cha
juu kidogo. Hii itakusaidia kujua soko la ajira na thamani yako.
Isiwe sawa kila
wakati
CV yako inabidi
iwe inaendana na kazi unayoomba. Hivyo basi wakati unaomba kazi tofauti kwa
kutumia CV ile ile ni vizuri ukajaribu kuiweka CV ikaendana na nafasi
unayoomba.
Usikate
tamaa
Tumia CV yako
kuitwa kwenye usahili. Huko utapata fursa ya kuelezea mafanikio yako.
Kitu cha muhimu,
USIKATE TAMAA! Kwa kila CV 100 unazotuma unaweza kuitwa kwenye usahili mara 10,
na katika mara kumi hizi utapata kazi moja tu- kazi yako ipo inakusubiria. Kua
makini na mwenye malengo na muda si mrefu utakua mmoja ya watu katika dunia ya
kazi.
v
0 comments:
POST A COMMENT