Wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi iliyoko katika halmashauri mjini wa Bariadi Mjini Bariadi wakiandamana katikati ya barabara kuu ya Bariadi-Lamadi, mjini Bariadi wakishinikizwa kurudishwa Mkuu wa shule yao ambaye alikuwa amepewa uhamisho Deus Toga, ambapo alikuwa amepelekwa shule ya sekondari Giriku na kuletewa Mkuu wa shule mwingine Paul Lutema ambaye walimkataa. |
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwa tayari kuzuia maandamano hayo. |
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwakamata baadhi ya wanafunzi wakati wa maanadamano hayo |
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwakamata baadhi ya wanafunzi wakati wa maanadamano hayo. |
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakimkamata mmoja wa wanafunzi wakati wa maanadamano hayo, ambapo walimkamata na kkumuweka kwenye gari la polisi. |
skari wengine wakiwakimbiza wanafunzi ili kuwakamata |
Akari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwa katika eneo la shule ya sekondari Bariadi, kuhakikisha wanafunzi wanaingia madarasani ili wasiendeleze maandamano. |
wanafunzi hao wakiwa wanaandamana, barabara kuu ya bariadi-lamadi |
ZAIDI ya Wanafunzi 600 wa shule ya sekondari ya Bariadi halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wameandamana na kufunga barabara kuu ya Bariadi –Lamadi kupinga kuhamishwa kwa mkuu wa shule hiyo Deus Toga.
Wanafunzi hao walianza kuandamana kwenda katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri,lakini ilishindikana baada ya kikosi cha jeshi la polisi kuzuia ghasia (FFU) kuwazuia kwenda katika ofisi hizo.
Hata hivyo wanafunzi hao wakiwa katikati ya barabara hiyo waliamua kuandamana tena kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa jambo lililoshindikana pia baada ya askari hao kuwazuia tena eneo la Hospitali teule ya mkoa (somanda).
Baada ya hali hiyo wanafunzi hao ambao ni kidato cha kwanza hadi cha sita waliamua kukaa katikati ya barabara huku wakimba nyimbo za kushinikiza kuwa hawamtaki mwalimu Paul Lutema ambaye alikuwa amepelekwa kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.
“hatumtaki mwalimu Lutema……tunamtaka mwalimu wetu Toga…..hatumtaki Lutema……Tunamtaka mwalimu Toga”
Wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kumkataa mwalimu Lutema na kumtaka mwalimu Deus Toga wanafunzi hao walianza kuwarushia mawe askari hao wakitaka wasiwazuie kwenda kofisi ya mkuu wa mkoa.
Baada ya hali hiyo jeshi la polisi walianza kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao huku wakiwafukuza kurejea katika eneo la shule ambapo baadhi yao walikamatwa na kupigwa virungu na kuwekwa ndani ya magari ya polisi hadi kupelekwa kituo cha polisi Bariadi.
“toka mwalimu huyu kafika shuleni hapa ufauru umeongezeka na migogoro ya shule iliyokuwepo haipo tena,na duka la shule lilikuwa limefungwa kutokana na migogoro ya walimu lakini toka amekuja hiyo migogoro imekwisha na duka linafanya kazi’’Alisema Justine Mshana.
ahsante kwa kutembelea blog hii
Great site for these post and i am seeing the most of contents have useful for my Carrier.Thanks to such a useful information.Any information are commands like to share him.
ReplyDeleteFresher Jobs in Chennai
Fresher Jobs in Delhi
Fresher Jobs in Bangalore
Fresher Jobs in Kolkata