KUJIONDOA KATIKA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO | MASWAYETU-BLOGSPOT
Breaking News
Loading...

Tuesday, February 7, 2017

KUJIONDOA KATIKA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO

BONYEZA HAPO CHINI KUJUA KUHUSU LINI AJIRA ZA WALIMU 2015/2016 ZITATOKA
Ndugu wanachama wa chama cha ACT-WAZALENDO,WATANZANIA kwa ujumla wenu leo tar 7/02/2017 niamua kujiondoa ramsi katika chama hiki cha ACT pasiko kushinikizwa na mtu wa kikundi chochote. Ni uamuzi wangu mwenyewe niliomua ili kuweza kupata muda mrefu wa kusimamia shughuli zangu binafsi zilizonibana kwa sasa.

ndugu watanzania wenzangu na wana songwe kwa ujumla napenda kuwapongeza na kuwashukuruni wale wote tuliokuwa tunashirikia ktk kipindi chote cha uongozi wangu kuanzia ngazi ya wilaya mpaka hii nilionayo sasa ya KATIBU wa mkoa wa songwe na imani tulikuwa ktk nia moja ya kupata mabadiliko makubwa ktk nchi yetu yenye kuleta usawa kwa kila mtanzania bila kujali CHEO,ITIKADI WALA JINSIA LANGO NI KUIWEKA NCHI YETU KATIKA HALI YA UTULIVU,UADILIFU NA KUTAWALIKA, pia niwapongeze viongozi na wanachama wa vyama vyote vya upinzani na tawala kwa ushirikiano wao mkubwa walionyesha kwangu kwa kipindi chote cha uongozi wangu!

Ndugu zangu naondoka ACT-WAZALENDO nikiwa nimekiacha mahala salama na penye hatua kubwa pia nawapongeza kwa mawazo yao waliokuwa nayo. Mimi kama mtanzania nchi yenye uhuru wa hali ya juu nimechukua maamuzi haya baada ya kuona juhudi na mawazo ya MH MAGUFURI ndio hayo tulikuwa tunayalilia watanzania wote siku zote na nitaonekana wa ajabu kuwa mtu wa kupinga au kudharau kwa sasa juhudi zinazofanywa na na MH RAIS kwa sasa mbele ya watanzania waliowanyonge walikuwa wanatamani ufisadi uonevu viondoke ndani ya nchi yetu nzuri ya TANZANIA hakika hivi vyote sasa kwa serikali hii ya awamu ya 5 juhudi za kuviondoa na kuwa weka watanzania katika hali ya usawa vinaonekana

Ninaondoka kama nilivyojiunga chama cha ACT kwa hiari yangu baada ya kuchoshwa na siasa za UONGO,UZUSHI na uchonganishi kwa watanzania wenzangu.

Kwa hiari yangu nimeamua kuyaenzi maneno ya marehemu babu yangu mbunge wa kwanza wilaya ya mbozi MZEE NICOLAUS NZUNDA alinitaka kufanya siasa safi ili wanyongr wenzangu wanikumbuke na kuniombea pale mwenyezi mungu ataponihitaji mja wake na hii ndio ilikuwa imani yangu na imani hii sasa kwangu inatuma kuukumbuka msemo wa USHIRIKA NI KAMA KOTI LIKIKUBANA LIVUE nami nalivua koti hili la ushirika wa ACT-Wazalendo kwa sasa halinitoshi na binasfi naamini si kosa kurudi NYUMBANI kule nilikowaacha wenzangu.

Natangaza rasmi kulejea chama changu kilichoasisiwa na wazee wetu walipigania TAIFA langu la TANZANIA narudi CCM nikiwa kichwa chini kwa kuona aibu kwa uongo tulikuwa kuwa tunakaa chini kukizushia na kuwadanganya watanzania.

Mwisho nawatakia kila la heri wale wote waliamua kuendelea kuwadanganya watanzania ambao leo wamebaini uongo huwa na kuonyesha kwa vitendo katk chaguzi zilizofanyika hapa karibuni maeneo mbali mbali ya nchi yangu.
 
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU UBARIKI MKOA WANGU WA SONGWE

AKSANTENI

RAHIM NZUNDA
KATIBU ACT MKOA WA SONGWE.

   Picha na Gaspal Simon Mazengo.
    "MASWAYETU BLOG TEAM"

Jiunge nansi upate taarifa moto moto na zenye uhakika. Zinazojili nchini kote v

google+

linkedin

About Author
  • Donec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Sed posuere consecteturDonec sed odio dui. Duis mollis, est non commodo luctus, nisi erat porttitor ligula, eget lacinia odio sem nec elit. Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT

     


    Travel

    About Us