Mauaji
ya kutumia silaha za moto yameendelea kushamiri nchini,baada ya
mfanyabiashara mmoja mjini Singida kufariki dunia baada ya kupigwa
risasi ya bunduki aina ya bastola wakati akitaka kuondoka dukani kurejea
nyumbani.
Mfanyabiashara huyo na mkazi wa Itungukia tarafa ya Mungumaji manispaa Singida ni Simon Charles (49).
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa jeshai la polisi mkoa
wa Singida,ACP Debora Magiligimba, alisema tukio hilo la kusikitisha
limetokea Aprili, 20 mwaka huu saa 3.30 usiku.
Alisema
siku ya tukio baada ya mfanyabiashara huyo kufunga duka lake la madawa
ya binadamu lililopo standi ya zamani ya mabasi alianza kuelekea kwenye
gari lake ili aweze kurejea nyumbani kwake.
“Wakati
akikaribia gari lake ghafla muuaji huyo ambaye alijificha upande
mwingine wa gari hilo alinyanyuka na kumpiga risasi titi la upande wa
kulia na kutokea nyuma na kisha kudondoka pale pale. Wasamaria wema
waliweza kumkimbiza hospitali ya mkoa lakini alifariki akipatiwa
matibabu.Kifo chake kinatokana na kuvuja damu nyingi,” alisema Magiligimba.
Kamanda
huyo alisema kwenye eneo la tukio kulipatikana ganda moja la risasi ya
bastola. Hadi sasa chanzo cha mauaji hayo, bado hakijajulikana.
Katika
hatua nyingine, Magiligimba alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na
msako mkali kubaini watu waliojihusisha na tukio hilo ili waweze
kukamatwa na sheria ziweze kuchukua mkondo wake.
“Jeshi
la polisi linatoa wito kwa wananchi wote mkoani kutoa ushirikiano kwa
jeshi hilo ili kusaidia kukamatwa kwa wauaji hao. Pia wafanyabiashara
tunawakumbusha umuhimu wa kuajiri walinzi, watakaowalinda wao na mali
zao,” alisisitiza.
Habari
kutoka eneo la tukio, zinaeleza kwamba mfanyabiashara huyo ambaye
kitaaluma ni daktari wa binadamu ameauwa na mtu mmoja ambaye alivalia
suruali. Baada ya mauaji hayo, mtu huyo aliondoka kwa miguu na kutokomea
kusiko julikana.
Mashuhuda
wengine wanadai kuwa muuaji huyo hakuweza kukamatwa wala kufukuzwa, kwa
madai kuwa mlio wa risasi ya bastola haukuwa mkubwa hivyo wakahisi kuwa
ni tairi la pikipiki limepasuka na hivyo walipuuzia.
picha na Gaspal simon mazengo
maswayetu term 2017
v
0 comments:
POST A COMMENT